Thursday, June 8, 2017

DIRECT PAY ONLINE GROUP [DPO] MDHAMINI WA KILIFAIR 2017 DARAJA LA PLATINAMU

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Direct Pay Online Group, Eran Feinsten (kushoto) jinsi wanavyotumia mfumo wa mawasiliano kutuma na kupokea fedha katika banda la kampuni hiyo katika maonesho ya Utalii na Viwanda ya Kili Fair yaliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi katikati ni Mkuu wa wilaya ya Moshi, Kippi Warioba.

Waziri wa Maliasili na Utalii,Profesa Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza na maafisa wa kampuni ya Direct Pay Online, Kate Gathii (kushoto) ambaye ni Mkuu wa Masoko na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Eran Feinsten (wa pili kushoto) alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonesho ya Utalii na Viwanda ya Kili Fair yaloyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi kuanzia taerehe 2 Juni, wengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii (TTB) Jaji Mstaafu Thomas Mihayo na Mkuu wa wilaya ya Moshi, Kippi Warioba.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kulia) akikaribishwa na Mkuu wa Masoko wa kampuni ya Direct Pay Online, Kate Gathii (kushoto) alipotembelea banda la kampuni hiyo ambao ni platnimu sponsor wa maonesho ya Utalii na Viwanda ya Kili Fair yaliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi kuanzia tarehe 2 June. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo,Eran Feinsten,wengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii (TTB) Jaji Mstaafu Thomas Mihayo na Mkuu wa wilaya ya Moshi, Kippi Warioba.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Direct Pay Online Group,Eran Feinsten (kushoto) akionesha namna wanavyotumia mfumo wa mawasiliano kutuma na kupokea fedha katika banda la kampuni hiyo katika maonesho ya Utalii na Viwanda ya Kili Fair yalioyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi kuanzia tarehe 2 mpaka tarehe 4 Juni. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii(TTB)Jaji Mstaafu Thomas Mihayo na Mkuu wa wilaya ya Moshi, Kippi Warioba.


DIRECT PAY ONLINE GROUP [DPO] MDHAMINI WA KILIFAIR 2017 DARAJA LA PLATINAMU

     Direct Pay Online Group ni mdhamini daraja la Platinamu katika KiliFair 2017
 DPO ni moja ya kampuni inayoongoza katika malipo Afrika ikiwa na operesheni nchini Kenya, Uganda, Rwanda, Tanzania, Zanzibar, Zambia, Namibia, Botswana na Afrika Kusini.

DPO imekuwa na bidhaa muhimu hasa: Programu za malipo ya mtandaoni kwa njia ya simu kama DumaPay na Marketplace [ambayo ni huduma ya bure kwa wafanyabiashara wanaofanyakazi na Direct Pay Online na pia kuna punguzo la gharama kwa asilimia 20 

HABARI KAMILI-----

 Shirika linaloongoza katika kutoa huduma za malipo Direct Pay Online ni mdhamini wa maonyesho makubwa ya utalii na biashara kanda ya Afrika Mashariki ya KILIFAIR 2017. Maonyesho hayo yaliyofanyika katika uwanja wa Ushirika tarehe 2 hadi 4 mwezi Juni mwaka huu yalikusanya wafanyabiashara zaidi ya 300 kutoka Tanzania na nchi jirani na kuwa na wageni zaidi ya 3000 kutoka nje na ndani ya nchi.

“Tunajivunia kuwa wadhamini wa kiwango hiki cha platinamu katika maonyesho makubwa kama haya. Hii ni fursa muhimu kwa kampuni yetu ya DPO kujitangaza kwa kazi kubwa tunayofanya ya kurahisisha malipo haswa kwa sekta ya safari,” alisema Mkurugenzi Mkuu wa DPO Eran Feinstein.

Katika bidhaa zilizokuwa katika maonyesho kwende banda la DPO ni pamoja na huduma ya bure inayoitwa MarketPlace ambayo iko wazi kwa wafanyabiashara na wateja wote wa hoteli, safari, mawakala na maduka wa DPO wanaotumia tovuti hiyo na huduma nyingine kuuza bidhaa zao na pia kuwapatia fursa ya kujitangaza ulimwenguni bure. DPO pia ilionyesha jinsi ya kutumia programu ya DumaPay ambayo inawezesha wafanyabiashara kuwatoza wateja wao kutumia teknolojia inayosoma kadi kwa usalama mahali popote na muda wowote. Mteja huweza kulipa kupitia kadi au simu kwa sarafu wanayopendelea.


Fahamu zaidi Kuhusu Direct Pay Online 

DPO (www.directpay.online​) ni kundi la makampuni linaloongoza katika kutoa suluhisho za malipo ya mitandaoni katika Afrika. Inatoa huduma kwa maelfu ya wafanyabiashara wa mitandaoni katika Afrika Mashariki, Kati na Kusini. DPO ilinunua kampuni ya PayGate ya Afrika Kusini https://www.paygate.co.za Septemba 2016 na VSC Namibia na Botswana Machi 2017 http://website.vcs.co.za/

DPO kwa sasa inahudumia zaidi ya wateja 20,000 barani Afrika ikiwemo mashirika ya ndege 50, maelfu ya mahoteli, mawakala wa usafiri na wafanyabiashara wengine wa mitandaoni na inaendelea kujitanua katika maeneo mapya. DPO inachukua kadi zote kubwa za malipo ikiwemo, malipo ya pesa kwa simu na pochi za mitandaoni (e-wallet) na ni kiongozi katika teknolojia, utoaji huduma kwa urahisi na usalama. Ni mtoa huduma hizi pekee katika Afrika Mashariki yenye hati ya viwango vya juu ijulikanayo kama PCI DSS Level 1, ikiwa ni shahada ya juu kabisa katika masuala ya usalama katika malipo ya kadi ikihakikisha viwango vya juu kabisa vya usalama na usiri wa data za watumiaji.

Mawasiliano:
DPO Group
Kate Gathii

kate@directpay.online

No comments: